Nafasi mpya za kazi TAMISEMI Kada ya Afya na Uwalimu-millkun - Millkun

Nafasi mpya za kazi TAMISEMI Kada ya Afya na Uwalimu-millkun

Nafasi mpya za kazi TAMISEMI
Nafasi mpya za kazi TAMISEMI

Nafasi mpya za kazi TAMISEMI Kada ya Afya na Uwalimu-millkun; Tangu mwaka 1961 hadi sasa  Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea, Wizara chini  ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye Ofisi ya Rais kama ilivyo sasa. Uamuzi  wa wapi inawekwa umekuwa ukifanyika ili kuimarisha utendaji wa Ofisi  hii.

Ofisi ya Rais TAMISEMI ni Wizara pekee ambayo Makao Makuu  yake yalianzia Jijini Dodoma tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini tangu  Serikali ilipotangaza Makao Makuu ya Serikali kuwa ni Dodoma na kwa Dar  es salaam kumekuwa na Ofisi ndogo. Uwepo wa Makao Makuu Dodoma ulikua na  lengo la kutoa fursa sawa kwa wadau wake wakuu hususan Mikoa na Mamlaka  za Serikali za Mitaa kufika Dodoma kwa urahisi wanapofuata huduma  mbalimbali.

Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka  Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Sura ya 8, Ibara ya 145 na  146. Upelekeaji wa madaraka kwa wananchi unapitia katika Mamlaka za  Serikali za Mitaa na ndiyo maana Serikali za Mitaa na ushirikishwaji wa  Wananchi katika mchakato wa maendeleo vimetambuliwa katika Katiba na  Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati Nchi yetu inapata  uhuru wake kulikuwa na majimbo kumi ya Utawala ambayo yaliritihiwa toka  utawala wa kikoloni wa Kiingereza mwaka 1966. Rais wa kwanza Hayati  Julius Kambarage Nyerere kwa Mamlaka aliyopewa aliunda Mikoa 15 na  kuondoa utaratibu wa mgawanyo wa nchi katika Majimbo. Hadi Sasa Nchi  yetu ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956,  Vijiji 12,319, Vitongoji 64,384 pamoja na Mitaa 4,263. Baada ya uhuru  Halmashauri zilikuwa jumla 45 na hadi kufikia mwaka 2009 zilikuwa  Halmashauri 129 na zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 184 mwaka 2021.

Nafasi mpya za kazi TAMISEMI
Nafasi mpya za kazi TAMISEMI

Also read New job opportunities at Jiteng Consultancy Limited

VIGEZO NA SIFA ZINAZO HITAJIKA

Bonyeza link hapo chini kuangalia vigezo vinavyo hitajika;

https://www.tamisemi.go.tz/announcement/tangazo-la-ajira-ualimu-na-afya-tamisemi-aprili-2023

Jinsi ya kutuma maombi na ku Apply

Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi
kwa nafasi za Kada za Afya na Elimu, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au wasiliana
na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026
2160210 au 0735 160210.