Nafasi mpya za kazi TAMISEMI Kada ya Afya na Uwalimu-millkun; Tangu mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea, Wizara chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kwenye Ofisi ya Rais kama ilivyo sasa. Uamuzi wa wapi inawekwa umekuwa ukifanyika ili kuimarisha utendaji wa Ofisi hii.
Ofisi ya Rais TAMISEMI ni Wizara pekee ambayo Makao Makuu yake yalianzia Jijini Dodoma tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini tangu Serikali ilipotangaza Makao Makuu ya Serikali kuwa ni Dodoma na kwa Dar es salaam kumekuwa na Ofisi ndogo. Uwepo wa Makao Makuu Dodoma ulikua na lengo la kutoa fursa sawa kwa wadau wake wakuu hususan Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufika Dodoma kwa urahisi wanapofuata huduma mbalimbali.
Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146. Upelekeaji wa madaraka kwa wananchi unapitia katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na ndiyo maana Serikali za Mitaa na ushirikishwaji wa Wananchi katika mchakato wa maendeleo vimetambuliwa katika Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati Nchi yetu inapata uhuru wake kulikuwa na majimbo kumi ya Utawala ambayo yaliritihiwa toka utawala wa kikoloni wa Kiingereza mwaka 1966. Rais wa kwanza Hayati Julius Kambarage Nyerere kwa Mamlaka aliyopewa aliunda Mikoa 15 na kuondoa utaratibu wa mgawanyo wa nchi katika Majimbo. Hadi Sasa Nchi yetu ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,384 pamoja na Mitaa 4,263. Baada ya uhuru Halmashauri zilikuwa jumla 45 na hadi kufikia mwaka 2009 zilikuwa Halmashauri 129 na zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 184 mwaka 2021.
Also read New job opportunities at Jiteng Consultancy Limited
VIGEZO NA SIFA ZINAZO HITAJIKA
Bonyeza link hapo chini kuangalia vigezo vinavyo hitajika;
https://www.tamisemi.go.tz/announcement/tangazo-la-ajira-ualimu-na-afya-tamisemi-aprili-2023
Jinsi ya kutuma maombi na ku Apply
Ili kupata maelezo ya kina kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi
kwa nafasi za Kada za Afya na Elimu, tafadhali bofya: www.tamisemi.go.tz au wasiliana
na Kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026
2160210 au 0735 160210.