KUONGEZA MUDA WA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU NCHINI KWA PROGRAMU AMBAZO BADO ZINA NAFASI KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024

KUONGEZA MUDA WA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA;Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya Tanzania kuwa udahili katika awamu zote tatu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu
nchini kwa mwaka wa masomo 2023/2024 umekamilika.

Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Tatu yanatangazwa na vyuo husika.

KUONGEZA MUDA WA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA
KUONGEZA MUDA WA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA

WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Tatu na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja wapo kuanzia leo tarehe 13 hadi 24Oktoba, 2023 kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili
ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.
Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili.

Orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja imewekwa kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).

KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA NNE YA UDAHILI

Baada ya kukamilika kwa awamu zote tatu za udahili, Tume imepokea maombi ya kuongezwa muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.

Hivyo, Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Nne na ya mwisho ya udahili inayoanza leo tarehe 13 hadi 17 Oktoba, 2023. Tume inasisitiza kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakufanikiwa kudahiliwa katika awamu zilizopita kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma kwa usahihi maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.

Tume inaelekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazofanya udahili wa Shahada ya Kwanza kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.

UTARATIBU WA UDAHILI KATIKA AWAMU YA NNE

Waombaji wa udahili na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa Awamu
ya Nne kama ilivyoainishwa katika Jedwali.

TAHADHARI

TCU inawaasa wananchi kuepuka kutapeliwa na watu wanaojiita mawakala au washauri
wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na vyuo vya Elimu ya Juu hapa nchini.

Leave a Comment