Nafasi Mpya za Kazi Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Nafasi Mpya za Kazi Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ni Shirika la umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya Mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019. Historia inaonyesha kuwa, Sheria ya kuunda upya Baraza hili ilifanywa kwa kuunganishwa Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya Mwaka 1974 na Baraza la Muziki la Taifa (BAMUTA) ya Mwaka 1974. Baraza liliundwa ili lisimamie maendeleo ya sanaa nchini

Kazi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Kwa mujibu wa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 5 ya Mwaka 2019, ambayo kwayo Baraza liliundwa, Majukumu ya Baraza ni pamoja na :

  • Kufufua na kuhimiza maendeleo ya kazi za Sanaa
  • Kufanya tafiti wa masuala mbalimbali ya Sanaa
  • Kutoa ushauri na misaada ya kitaalamu kwa asasi au watu wanaojihusisha na shughuli za sanaa.
  • Kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu au Taasisi mbalimbali
  • Kutoa na kuimarisha mipango ya mafunzo kwa Wadau wa Sanaa
  • Kuishauri Serikali juu ya mambo yahusuyo maendeleo na uzalishaji wa kazi za Sanaa.
  • Kuhamasisha maendeleo ya Sanaa kwa njia ya Maonyesho, Mashindano, Matamasha, Warsha na Semina.
  • Kuanzisha, kukusanya na kuhifadhi torwi, ikiwa pamoja na zile zinazohusu watu, Asasi, Taasisi, vifaa na miundo mbinu inazohusiana na Sanaa
  • Kusajili Wasanii na wale wote wanaojihusisha na shughuli za Sanaa.

 

Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA)Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA)
Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA)

Muundo wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Baraza la Sanaa la Taifa lina wajumbe wa Baraza ambao huteuliwa na Waziri anayehusika na masuala ya Sanaa. Mwenyekiti wa Baraza huteuliwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Baraza huteuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu. Wakati ambapo vipindi vya kuteuliwa kwa wajumbe havina ukomo, uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza ni kwa vipindi viwili tu vinavyofuatana. Kwa kawaida wajumbe wa Baraza huteuliwa kwa msingi wa uwakilishi wa mikoa, asasi, asasi zinazofundisha Sanaa, idara za Serikali na asasi zisizo za Serikali.

 

Baraza linaongozwa na Katibu Mtendaji, ambaye ndiye Afisa mtendaji mkuu. Baraza lina idara Mbili zifuatazo:

  • Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa, inayohusika na huduma za Sanaa
  • Idara ya Huduma ya Taasisi, inayohusika na shughuli za huduma za Taasisi

 

Licha ya idara hizo Mbili, kuna vitengo vitano ambavyo hufanya kazi moja kwa moja chini ya Katibu Mtendaji. Vitengo hivyo ni ;

  • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
  • Kitengo cha Manunuzi
  • Kitengo cha Habari na Mawasiliano
  • Kitengo cha Sheria
  • Kitengo cha Tehama na Takwimu
Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA)Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA)
Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA)

KITENGO CHA KAZI

AFISA SANAA DARAJA LA II – 4 POST

MUDA WA KUJISAJILI KATIKA NAFASI HIYO

2022-09-01 2022-09-14

MAJUKUMU YA NAFASI HIYO

i.Kutafsiri, kukagua na kufuatilia ubora na miiko ya kazi za muziki au uandaaji wa muziki.

ii.Kuandaa na kupokea namna nzuri ya kutengeneza muziki kupitia midia mbalimbali mfano you tube.

iii.Kusimamia na kushiriki katika matukio ya muziki.

iv.Kutembelea na kukutana na wachoraji, wachongaji na kubadilishana uzoefu.

v.Kutafsiri, kukagua huduma bora na miiko ya uchoraji, uchongaji na sanaa za maonyesho.

vi.Kuhudhuria matamasha mbalimbali yahusuyo uchoraji, uchongaji na sanaa za maonyesho.

vii.Kufanya shughuli nyinginezo zitakazopangwa na mkuu wa kazi.

i.Kutafsiri, kukagua na kufuatilia ubora na miiko ya kazi za muziki au uandaaji wa muziki.

ii.Kuandaa na kupokea namna nzuri ya kutengeneza muziki kupitia midia mbalimbali mfano you tube.

iii.Kusimamia na kushiriki katika matukio ya muziki.

iv.Kutembelea na kukutana na wachoraji, wachongaji na kubadilishana uzoefu.

v.Kutafsiri, kukagua huduma bora na miiko ya uchoraji, uchongaji na sanaa za maonyesho.

vi.Kuhudhuria matamasha mbalimbali yahusuyo uchoraji, uchongaji na sanaa za maonyesho.

vii.Kufanya shughuli nyinginezo zitakazopangwa na mkuu wa kazi.

SIFA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA

Mhitimu wa Shahada ya kwanza kati ya Taaluma zifuatazo;- Muziki, Sanaa za Maonyesho, Filamu, Mitindo Filamu na Televisheni kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

Login to Apply

Leave a Comment